Msichana wa umri wa miaka mitatu auawa na tembo Mkoani Simiyu,Tanzania
2021-10-01 10:01:10| cri

Mtoto Agnes Charles mwenye umri wa miaka mitatu amekufa baada ya kuangukiwa na matofali akiwa amelala baada ya nyumba yao kubomoka wakati tembo wakitaka kuingia ndani kula viazi vikavu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika nyumba yao.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,  Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Septemba 29, 2021 saa mbili usiku katika kijiji cha Mwanzagamba wilayani Meatu. Amesema tembo wawili walivamia makazi, watu na kuvunja nyumba ambayo mtoto alikuwa amelala, na pia kulihifadhiwa chakula ambacho tembo walikuwa wanakitafuta.