Biashara ndani ya kanda ya Afrika Mashariki yashuka kwa asilimia 5.5 kutokana na COVID-19
2021-10-01 09:37:05| CRI

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limesema biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeshuka kwa asilimia 6.6 ma kufikia dola za kimarekani bilioni 5.9 mwaka jana kutokana na janga la virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa katika semina iliyoendeshwa kwa njia ya mtandao kuhusu Kufufua Uwekezaji na Biashara wakati wa janga la COVID-19.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo John Bosco Kalisa amesema, sekta binafsi ni muhimu katika ajenda ya kuchochea ufufukaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wakati huu wa janga la COVID-19.

Mkurugenzi wa sekretarieti ya Biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Rashid Kibowa amesema, janga hilo limeathiri utendaji wa biashara, na kuongeza kuwa, uagizaji wa bidhaa kwa kanda hiyo ulishuka na kufikia dola bilioni 3.56 za kimarekani mwaka 2020 kutoka dola bilioni 3.95 mwaka 2019.