Zaidi ya familia 100 zakosa nyumba za kukaa baada ya upepo mkali kubomoa nyumba zao mkoani Rukwa Tanzania
2021-10-04 09:45:23| cri

Zaidi ya familia 100 zimekosa nyumba za kukaa baada ya nyumba 30 kubomoka kutokana na upepo mkali uliotokea Jumamosi jioni mkoani Rukwa Tanzania.

Diwani wa Kata ya Mkale Alfred Mpandashalo amesema familia zimeachwa zikiwa hazina makaazi baada ya vijiji vya Usevya na Mkole Wilaya ya Kalambo kukumbwa na upepo mkali ulioezua mapaa na kusababisha kuta za nyumba kuanguka. Watu hao wamelazimika kuhama na kutafuta hifadhi kwa majirani zao.

Diwani Mpandashalo ameitaka serikali na wasamaria wema kuzichangia familia zilizoathirika wakati mamlaka zinatathmini hasara iliyosababishwa na upepo huo.