Askari mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ashambuliwa na kuuawa kaskazini mashariki mwa Mali
2021-10-04 09:44:25| cri

Askari mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ashambuliwa na kuuawa kaskazini mashariki mwa Mali_fororder_2

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali tarehe 2 ilitoa taarifa ikisema askari mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa aliuawa kwenye shambulizi la mlipuko lililotokea jimbo la Kidal, kaskazini mashariki mwa Mali.

Taarifa hiyo imesema msafara wa magari ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliofanya operesheni karibu na mji wa Tessalit jimboni Kidal ulishambuliwa kwa mabomu tarehe 2, ambapo askari mmoja aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya. Uraia wa askari hao haukutajwa kwenye taarifa hiyo.