Iran yalitaka shirika la IAEA kueleza wazi msimamo wake juu ya tukio la kuharibu vifaa vya nyuklia vya Iran
2021-10-04 09:43:57| cri

Iran yalitaka shirika la IAEA kueleza wazi msimamo wake juu ya tukio la kuharibu vifaa vya nyuklia vya Iran_fororder_3

Kiongozi wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) Bw. Mohammad Eslami jana alisema Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) lazima lieleze wazi msimamo wake juu ya kitendo cha kuharibu jengo la AEOI mwezi Juni.

Akizungumza na wanahabari Bw. Eslami amesema ni muhimu kutambua kwamba tukio la ugaidi lilitokea huko, na Israel imethibitisha pia. Akijibu swali kuhusu matakwa ya wasimamizi wa mambo ya nyuklia wa Umoja wa Mataifa ya kuangalia kamera ya uchunguzi, amesema Iran haina wajibu wa kuwaruhusu kufanya hivyo.