Kenya yaadhimisha Siku ya Makazi Duniani ikifuata wito wa miji inayokua kwa kasi bila ya uchafuzi
2021-10-05 10:27:04| CRI

Kenya yaadhimisha Siku ya Makazi Duniani ikifuata wito wa miji inayokua kwa kasi bila ya uchafuzi_fororder_22

Kenya Jumatatu iliadhimisha Siku ya Makazi Duniani ikifuata wito mpya wa miji mikubwa na midogo inayokua kwa kasi bila ya uchafuzi kupitia usimamizi bora wa taka na utoaji mdogo wa kaboni.

Maafisa wamesema serikali imeshirikiana na sekta binafsi kutekeleza mwongozo kabambe wa mazingira ya kijani ya miji na kuboresha afya pamoja na kuondoa athari za kiuchumi kwa wakaazi. Waziri wa Usafiri, Miundombinu, Nyumba na Maendeleo ya Miji, James Macharia amesema kukuza miji bila uchafuzi ni mwitikio wa msukosuko wa hali ya hewa.

Amesema kuanzisha upya maeneo ya mijini yasiyo na uchafuzi, kutunga sera na udhibiti wa mageuzi ili kuongeza kasi ya matumizi ya nishati mpya na utoaji sifuri wa uchafuzi vinalenga kuhimiza ubora wa hali ya hewa kwa jamii za wenyeji.