Takriban watu 37 wauawa katika mzozo wa kikabila jimboni Warrap nchini Sudan Kusini
2021-10-06 09:42:53| CRI

Takriban watu 37 wameuawa na wengine 48 kujeruhiwa katika siku tatu zilizopita kutokana na ghasia mpya zilizoibuka kati ya jamii katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini.

Naibu msemaji wa Huduma ya Polisi ya Kitaifa Bw. Dak Karlo amesema kuwa mapigano kati ya vijana wenye silaha yaliibuka Jumapili kati ya jamii za Luacjang, Yhhiik, na Lou-paher za kijiji cha Romathieng, Kaunti ya Tonj Mashariki.

Mgogoro kati ya koo umeibuka tena huko Warrap kutokana na wizi wa ng'ombe.

Alisema mamlaka za jimbo hilo zinafanya juhudi za kuimarisha hali ya usalama katika maeneo yaliyoathirika ili kudhibiti hali hiyo inayozidi kuzorota, akibainisha kuwa serikali itawachukulia hatua za kisheria wahalifu.