Mwanadiplomasia mwandamizi wa China kukutana na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani
2021-10-06 09:37:55| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying tarehe 6 ametangaza kuwa, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Yang Jiechi atakutana na Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Taifa wa Marekani Bw. Jake Sullivan mjini Zurich nchini Switzerland.

Hua amesema Yang Jiechi atakutana na Sullivan kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa China na Marekani walioongea kwa njia ya simu tarehe 10 mwezi Septemba. Yang na Sullivan watabadilishana maoni juu ya uhusiano kati ya China na Marekani pamoja na masuala husika.