Mjumbe maalumu wa China kwenye UM alihimiza baraza la usalama kujibu wasiwasi wa DRC juu ya vikwazo
2021-10-06 09:38:42| CRI

Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Dai Bing Jumanne alilihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lifuatilie wasiwasi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) juu ya vikwazo.

Dai amesema baraza la usalama linatakiwa kujibu wasiwasi ya DRC juu ya marekebisho ya hatua za vikwazo, ili kuepusha matokeo mabaya juu ya ujenzi wa uwezo wa mambo ya usalama nchini humo.

Dai pia ameisifu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuweka na kutekeleza mpango wa utekelezaji wa miaka mitatu, ambao unahudumu kama mwongozo wa amani ya kudumu na maendeleo endelevu kwa nchi hiyo. Amesema China inatarajia serikali ya DRC itatilia maanani kuhimiza mageuzi ya sekta muhimu na kuboresha uwezo wa utawala. China inaziunga mkono pande zote husika zifanye mazungumzo shirikishi, na kutatua tofauti kwa njia mwafaka chini ya mfumo wa katiba.