Maofisa waandamizi wa China na Marekani wakutana
2021-10-07 10:06:24| CRI

Maofisa waandamizi wa China na Marekani wakutana_fororder_33

Mshauri mwandamizi wa sera za kigeni wa China Yang Jiechi na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan wamekutana mjini Zurich, Uswisi, na kubadilishana maoni kwa kina juu ya uhusiano kati ya nchi hizi na masuala ya kimataifa na kikanda wanayoyafuatilia kwa pamoja.

Kwenye mazungumzo yao yaliyotajwa kama ni ya kiujenzi na kusaidia kuhimiza maelewano, maofisa hao walikubaliana kuwa China na Marekani zitachukua hatua, kufuata moyo wa mazungumzo ya simu yaliyofanywa na marais wao mwezi uliopita, kuongeza mawasiliano ya kimkakati, kushughulikia tofauti kwa mwafaka, kuepuka makabiliano na mgogoro, kutafuta matokeo yanayonufaisha pande zote mbili na kufanya kazi pamoja ili uhusiano kati ya China na Marekani urudi kwenye njia sahihi na maendeleo tulivu.

Yang pia amesisitiza msimamo wa China juu ya masuala yanayohusu Taiwan, Hong Kong, Xinjiang, Tibet, haki za binadamu na usafiri baharini, na kuitaka Marekani iheshimu mamlaka na maslahi ya usalama na maendeleo ya China na kuacha kutumia masuala hayo kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Kwa upande wake, Sullivan amesema Marekani inafuata sera ya kuwepo kwa China moja.