Bw. Guterres asema Ethiopia haina haki ya kuwafukuza wafanyakazi wa UM
2021-10-07 10:01:19| CRI

Bw. Guterres asema Ethiopia haina haki ya kuwafukuza wafanyakazi wa UM_fororder_22

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Ethiopia haina haki ya kuwafukuza wafanyakazi wa umoja huo na hicho ni kitendo kinachokiuka sheria ya kimataifa.

Akiongea moja kwa moja na mwakilishi wa kudumu wa Ethiopia kwenye UM, Taye Atske Selassie, ambaye pia alikuwepo kwenye Baraza la Usalama, Bw. Guterres amesema kama kuna waraka wowote wa maandishi, uliotolewa na serikali ya Ethiopia kwa taasisi yoyote ya UM kuhusu mfanyakazi yeyote kati ya hao waliofukuzwa, angependa kupokea nakala yake, kwani yeye hafahamu chochote. Pia amesema wako tayari kushirikiana na serikali ya Ethiopia kwenye suala lolote ambalo serikali hiyo inahisi kuwa wafanyakazi wa UM hawaoneshi moyo wa kutopendelea au moyo wa uhuru kama sheria ya kibinadamu inavyoelezea na kanuni za kibinadamu zinavyoonesha.

Wakati huohuo Bw. Guterres ameitaka serikali ya Ethiopia kuuruhusu umoja huo kuwasaidia mamilioni ya watu wenye uhitaji wa msaada wa kibinadamu.