Tanzania yapata mabehewa ya mizigo yaliyotengenezwa na China ili kuimarisha usafiri wa mizigo wa reli ya kati
2021-10-07 09:59:30| CRI

Shirika la Reli Tanzania (TRC) jana limepokea mabehewa mapya 44 ya mizigo yaliyotengenezwa na China, ambayo ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa usafiri wa mizigo wa reli ya kati nchini Tanzania.

Mkurugenzi mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema kila behewa linaweza kuchukua mizigo ya tani 46. Reli ya kati inayotoka bandari ya Dar es Salaam hadi magharibi na kaskazini mwa Tanzania ni njia muhimu kwa nchi zisizo na bahari, zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa amesema mikopo isiyo na masharti magumu ya Benki ya Dunia inafadhili mradi wa maendeleo ya reli wa Tanzania, ili kurekebisha njia ya reli ya kati.