Kenya yazindua makubaliano ya plastiki ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mzunguko
2021-10-08 09:52:43| CRI

Kenya imekuwa nchi ya pili katika Afrika baada ya Afrika Kusini na ya 12 duniani kuzindua makubaliano ya plastiki ambayo lengo lake kuu ni kuchochea ukuaji wa uchumi wa mzunguko kupitia kutumia tena taka zisizoweza kuoza.

Keriako Tobiko, waziri wa Mazingira na Misitu amesema mbali na kutoa fursa za ajira, uzinduzi wa mpango huo wa umma na binafsi wa kutengeneza upya taka za plasitiki na kuzitumia tena utashughulikia uchafuzi wa mijini. Inakadiriwa kuwa utahimiza usimamizi endelevu wa taka za plastiki ambazo zinachukua takriban asilimia 30 ya tani 22,000 za taka yabisi zinazotolewa nchini kila siku.

Uzinduzi huo umefanywa na Muungano wa Sekta Binafsi (KEPSA) ukishirikiana na Biashara ya Ushirikishwaji Endelevu (SIB), ambao pia umeidhinishwa na watengenezaji, wasimamizi na asasi za kiraia.