Mwandishi wa Tanzania Prof. Abdulrazak Gurnah ashinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021
2021-10-08 09:54:34| CRI

Mwandishi wa Tanzania Prof. Abdulrazak Gurnah ashinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021_fororder_22

Mwandishi wa Tanzania Prof. Abdulrazak Gurnah ametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Chuo cha Sweden kilisema tuzo hiyo ni kwa ajili ya kutambua mtazamo wake wa kutokubali na huruma yake juu ya athari za ukoloni.

Gurnah ambaye alizaliwa katika Kisiwa cha Zanzibar, na sasa anaishi Uingereza, ni profesa katika Chuo Kikuu cha Kent. Riwaya yake "Paradise" iliorodheshwa kwenye Tuzo ya Booker mwaka 1994.

Tuzo hiyo ya heshima inajumuisha medali ya dhahabu na kronor milioni 10 za Sweden ambazo ni sawa na dola za kimarekani zaidi ya milioni 1.14.