WHO yapanga kuchanja asilimia 40 ya watu wa kila nchi dhidi ya Corona mwishoni mwa mwaka 2021
2021-10-08 09:51:25| CRI

WHO yapanga kuchanja asilimia 40 ya watu wa kila nchi dhidi ya Corona mwishoni mwa mwaka 2021_fororder_33

Shirika la Afya Duniani (WHO) jana lilitangaza mpango wa kuchanja asilimia 40 ya watu wa kila nchi dhidi ya Corona hadi mwishoni mwa mwaka 2021 na asilimia 70 ifikapo katikati ya mwaka 2022, ikiweka kipaumbele kutoa chanjo za Corona kwa watu wa nchi zenye mapato ya chini hasa nchi za Afrika.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza na wanahabari amesema, WHO inaanzisha mkakati huo na ili kuweza kuutimiza zinahitajika angalau dozi bilioni 11 za chanjo, ambapo kuna tatizo la mgao na sio tatizo la utoaji. Kwa sasa, idadi ya uzalishaji wa chanjo za Corona imefikia takriban bilioni 1.5 kwa mwezi kote duniani, kama zitagawanywa kwa usawa, kutakuwa na usambazaji wa kutosha katika kutimiza lengo hilo.