Mkutano wa maadhimisho ya miaka 110 ya Mapinduzi ya Mwaka 1911 wafanyika Beijing
2021-10-09 12:31:14| Cri

Rais Xi Jinping wa China leo amehutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 110 tangu Mapinduzi ya mwaka 1911 na kuelezea tukio hilo la kihistoria lililotokea miaka 110 iliyopita inaonesha nini kwa watu wa China.

Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi amesema miaka 110 iliyopita imeonyesha kuwa ili kustawisha tena taifa, lazima kuwe na nguvu kubwa ya kuwaongoza watu wa China kusonga mbele, na nguvu hiyo ndio CPC. Amesema bila ya CPC, isingekuwepo China mpya wala ustawi wa taifa, akisisitiza juhudi za kuhakikisha Chama kinasimama kama uti wa mgongo wa kuaminika na taifa la China na watu.

Xi amesema miaka 110 iliyopita imeonyesha kuwa ili kutimiza ustawi wa taifa, njia inayofuata China ni muhimu sana. Ujamaa wenye umaalum wa kichina umethibitishwa kuwa ni njia sahihi pekee. 

Ameongeza kuwa China itahakikisha utekelezaji wa Mpango wa Kutafuta Maendeleo ya Sekta Tano kwa Uratibu na Mkakati Kamili wa Kazi Kuu Nne, kuimarisha mageuzi na kufungua mlango, kuboresha mfumo na uwezo wa kushughulikia mambo ya ndani kuwa wa kisasa, na kufanya kazi juu chini kutimiza matakwa ya watu ya kuwa na maisha bora, na kutimiza ustawi kwa wote.