Upotoshaji bado unakwamisha utoaji chanjo ya COVID-19 nchini Zambia
2021-10-11 08:50:01| CRI

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amezindua upya kampeni ya utoaji chanjo nchini Zambia ili kuwahimiza wananchi kupewa chanjo.

Rais Hichilema amezindua kampeni hiyo wakati Zambia imethibitisha kuwa upotoshaji bado ni tatizo kubwa linalofanya watu wakatae kupewa chanjo, na wakati nchi hiyo inatarajiwa kukumbwa na wimbi la tatu la maambukizi kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu Zambia ilipoanza kampeni ya kutoa chanjo, ni asilimia 5 tu ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanaotakiwa kupewa chanjo ndio wamepewa chanjo. Watu wenye umri huo ni asilimia 70 ya watu wanaotakiwa kupewa chanjo.

Kwenye mahojiano yaliyofanywa na watu mbalimbali mjini Lusaka yanaonesha kuwa bado watu wanauelewa mbaya kuhusu chanjo, licha ya uhamasishaji unaofanywa na mamlaka za afya.