Mkutano wa 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Bioanuwai kufunguliwa leo mjini Kunming, China
2021-10-11 08:34:51| CRI

Kipindi cha kwanza Mkutano wa 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Bioanuwai (COP 15) unafanyika kuanzia leo Oktoba 11 hadi 15 mjini Kunming, mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China.

Imefahamika kuwa mkutano huo wa COP 15 utafanyika kwa vipindi viwili, ambapo kipindi cha pili kitafanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022 kwa njia ya mtandao. Katika kipindi cha kwanza, mkutano huo unatarajiwa kupitia miswada mbalimbali isipokuwa ya “Mfumo wa Bioanuwai Duniani Baada ya Mwaka 2020”, ambayo itajadiliwa na kuamuliwa kwenye kipindi cha pili cha mkutano.

Ofisa habari wa Sekritarieti ya Mkataba wa Bioanuwai wa Umoja wa Mataifa Liu Sijia, amesema kati ya malengo 20 ya utekelezaji ya kuhifadhi bioanuwai yaliyowekwa mwaka 2010, ni malengo sita tu yamefikiwa kiasi, na hakuna hata lengo moja lililotimizwa kikamilifu. Kwa hiyo jumuiya ya kimataifa ina matarajio makubwa kwa “Mfumo wa Bioanuwai Duniani Baada ya Mwaka 2020”.