Viongozi wa Misri na Sudan Kusini wajadili uhusiano kati ya nchi zao na maswala ya kikanda
2021-10-11 09:19:32| CRI

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir jana walifanya mazungumzo wakijadili njia za kuimarisha uhusiano wa nchi zao katika mambo ya siasa, uchumi na usalama.

Rais al-Sisi alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo kuwa wanafuatilia matokeo ya duru ya kwanza ya mkutano wa kamati ya ushirikiano ya ngazi ya juu uliofanyika mwezi Julai mwaka jana, na fursa zilizoletwa kwa majadiliano. Pia walisaini makubaliano kuhusu umwagiliaji, biashara na viwanda.

Rais al-Sisi alisisitiza kuwa Misri itaendelea kuiunga mkono kithabiti Sudan Kusini na kufanya juhudi zake kuunga mkono njia zote za kuhimiza amani, utulivu na maendeleo nchini humo.