Katibu mkuu wa NRM Uganda: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itaifanya Dunia ishikamane zaidi
2021-10-11 09:47:33| CRI

Katibu mkuu wa NRM Uganda: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itaifanya Dunia ishikamane zaidi_fororder_Richard Awany Todwong

Katibu mkuu wa Chama tawala cha Uganda NRM Bw. Richard Awany Todwong, amesema China itaandaa kwa mara nyingine tena michezo ya Olimpiki itakayowaleta pamoja wanariadha wa nchi mbalimbali duniani, na kuifanya dunia ishikamane kwa karibu zaidi. Wakati huohuo, dunia pia inaweza kuielewa zaidi China kupitia michezo hiyo.

Bw. Todwong amesema hayo kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kwa njia ya mtandao. Amesema huu ni mwaka wa 50 tangu China irejeshewe kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa, katika miaka hiyo 50 iliyopita China siku zote imekuwa ni mshirika wa maendeleo wa Afrika, na katika kipindi ambacho nchi za Afrika zilikuwa zikipigania uhuru na ukombozi, China ilikuwa imesimama bega kwa bega na Afrika. Ameeleza imani yake kuwa katika siku zijazo China na Afrika hakika zitaendelea kukuza urafiki wao wa kihistoria.

Akizungumzia mustakbali wa ushirikiano kati ya China na Uganda, na kati ya China na Afrika kwa ujumla, Bw. Todwang anaona, chini ya mfumo wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, miundombiu ya Uganda, haswa ya barabara na nishati, imeboreka kwa kiasi kikubwa kutokana na msaada wa China. Lakini anaona bado kuna maeneo manne ambayo yanahitaji mkazo mkubwa zaidi kwenye ushirikiano huo:  Kwanza ni sekta ya kilimo, ambayo inatakiwa kukuzwa zaidi ili kutatua changamoto ya usalama wa chakula; Pili ni sekta ya uchumi na biashara, anatumia kuwa jumuiya za kibiashara za kikanda za Afrika ikiwemo jumuiya ya Afrika Mashariki EAC zitaongeza mawasiliano na ushirikiano wa kibiashara na China; Tatu ni sekta ya raslimali watu, ambayo Uganda inatarajia uungaji mkono mkubwa zaidi kutoka China; Nne ni sekta ya utalii, amewakaribisha watalii wengi zaidi wa China kuitembelea Uganda na nchi nyingine za Afrika, ili kuimarisha mawasiliano na maelewano kati ya pande hizo mbili.

Bw. Todwang amesema anatumai kuwa sekta hizo zitatiliwa maanani zaidi katika Mkutano ujao wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika nchini Senegal mwaka huu.