Tanzania yatenga dola milioni 157 za kimarekani kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
2021-10-12 09:19:32| CRI

Serikali ya Tanzania imetenga dola milioni 157 za kimarekani kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, na kupunguza madhara yake na kuzoea hali hiyo.

Waziri wa ofisi ya makamu wa rais wa Tanzania anayeshughulikia mambo ya muungano na mazingira Bw. Selemani Jafo, amesema miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na kujenga ukuta kwenye pwani ya bahari ya Hindi ili kupunguza mmomonyoko unaosababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari.

Bw. Jafo amesema kabla ya Mkutano wa 26 wa Mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa (COP26) utakaofanyika nchini Scotland, Tanzania itawasilisha ajenda saba katika mkutano huo, pamoja na kuisisitiza jumuiya ya kimataifa kutekeleza makubaliano kuhusu kupunguza athari ya mabadiliko ya tabia nchi.