Algeria yaahidi kuendelea kudumisha utoaji wa kuaminika wa mafuta kwa Ulaya
2021-10-12 09:54:38| CRI

Waziri wa nishati na madini wa Algeria Bw. Mohamed Arkab amethibitisha kuwa nchi yake itaendelea kudumisha utoaji wa mafuta wenye “uaminifu na wa uhakika” kwa Ulaya.

Waziri huyo amesema nchi yake ni mtoaji anayetegemeka wa gesi asilia, kwa sababu ina maliasili nyingi za gesi na kampuni ya taifa ya Sonatrach ni mzalishaji wa mafuta mzoefu na mwenye ufanisi.

Bw. Arkab amesema bomba la gesi la Medgaz linalounganisha Algeria na Hispania kupitia bahari, limehakikisha utoaji wa mita za ujazo bilioni 8 za gesi kila mwaka, huku akibainisha kuwa hadi kufikia mwezi Desemba uwezo wa bomba hilo utaongezeka hadi kufikia mita za ujazo bilioni 10.6.