Jimbo la Nigeria latafuta uwekezaji wa China katika sekta ya kilimo
2021-10-12 09:10:35| CRI

Jimbo la Bayelsa lililoko kusini mwa Nigeria limewaalika wawekezaji wa China kuwekeza katika sekta ya kilimo, ili kusaidia mpango wa maendeleo wa jimbo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu baada ya mkutano wa wikiendi uliofanyika Abuja na Balozi wa China nchini Nigeria Bw. Cui Jianchun, gavana wa jimbo la Bayelsa Douye Diri amesema jimbo lake limeitambua sekta ya kilimo kuwa sekta kuu ambayo itahimiza maendeleo endelevu na ukuaji.

Gavana huyo amesema China imerekodi mafanikio makubwa katika kuendeleza uchumi na kutokomeza umaskini, na iliahidi kushirikiana na nchi zinazoendelea ikiwemo Nigeria kupitia majukwaa kama vile “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kusaidia kupunguza umaskini. Gavana huyo amesema jimbo la Bayelsa linatoa dirisha kubwa kwa dunia, na pia litakuwa jukwaa zuri la kuonesha “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.