Mkutano wa COP15 watoa msisitizo kwenye suala ya ustaarabu wa kiikolojia
2021-10-12 11:04:31| CRI

Mkutano wa COP15 watoa msisitizo kwenye suala ya ustaarabu wa kiikolojia_fororder_1127946932_16339607898111n

Mkutano wa 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Viumbe anuwai (COP 15) umeanza jana mchana mjini Kunming, mkoa wa Yunnan kusini magharibi mwa China.

Mkutano huo wenye kaulimbiu “Ustaarabu wa Kiikolojia: Ujenzi wa Hatma ya Pamoja kwa Viumbe Hai Duniani,” ni wa kwanza kuandaliwa na Umoja wa Mataifa ukiwa na msisitizo wa ustaarabu wa kiikolojia.

Katibu Mtendaji wa Mkutano huo, Elizabeth Maruma Mrema amehudhuria mkutano huo na kusifia juhudi za China katika kuhifadhi anuwai ya viumbe. Amesema ili kutimiza lengo la mwaka 2050 la kuishi kwa masikilizano na asili, dunia inapaswa kuchukua hatua za kivitendo kaika muongo huu ili kurejesha anuwai ya viumbe na kuweka njia ya ufufukaji.

Naye msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi mtendaji wa Mradi wa Mazingira wa Umoja huo, Inger Andersen ametuma salamu zake za ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video, akisema kuwa na amani na asili ni kazi kuu ya karne ya 21, kwa kuwa asili ni msingi wa tamaduni, jamii, na uchumi wa binadamu wote.