Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya nishati ni muhimu kwenye kufufua uchumi baada ya COVID-19
2021-10-14 08:55:57| CRI

Wataalam waliohudhuria kongamano la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika lililofanyika mjini Nairobi, wamesema ushirikiano kwenye sekta ya nishati kati ya pande hizo mbili ni muhimu katika kufufua uchumi kutokana na madhara ya janga la Corona.

Kongamano hilo lililoitishwa na jumuiya ya washauri bingwa ya Afrika yenye makao yako mjini Nairobi na Taasisi ya Taifa ya China ya Shirika la Uchumi na teknolojia (CNPC-ETRI), lilihudhuriwa na watunga sera waandamizi, wanaviwanda watendaji na wanazuoni kutoka China na Afrika.

Katibu Mkuu wa Idara ya maendeleo ya viwanda ya Kenya Bw. Kirimi Kaberia amesema nchi za Afrika zinapenda kushirikiana zaidi na China ili kuwa na usalama wa nishati na kuwa na sekta yenye nguvu ya uzalishaji viwandani.

Konsela mkuu wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Yijun, amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika ili kulisaidia bara hilo kuwa na usalama wa mafuta na kuchochea ongezeko la sekta ya uzalishaji viwandani.