Uchumi wa Somalia waendelea kufufuka licha ya athari za COVID-19
2021-10-14 09:19:00| CRI

Benki kuu ya Somalia imesema uchumi wa nchi hiyo unatarajiwa kuongezeka hatua kwa hatua licha ya kuwepo kwa athari mbaya za janga la COVID-19 ambalo limeathiri sana ongezeko la uchumi katika robo ya tatu na ya nne ya mwaka 2020.

Benki hiyo imesema pato la taifa la Somalia linakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 2.4 katika mwaka 2021 kutokana na hatua za kuzuia janga la COVID-19, hatua za kupambana na nzige wa jangwani na ukame.

Benki hiyo imesema kiwango cha juu cha mfumko wa bei kimebaki kuwa chini ya asilimia 10 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, na  kiwango cha ubadilishaji wa fedha kimeendelea kuwa tulivu katika maeneo mengi ya Somalia.