Kenya yapanga kuongeza mapato ya kodi kwa kupunguza nakisi ya fedha
2021-10-14 09:26:24| CRI

Waziri wa fedha na mipango wa Kenya Bw. Ukur Yatani amesema Kenya ina mpango wa kuongeza mapato ya kodi ili kupunguza nakisi yake ya fedha kutoka asilimia 7.4 ya mwaka huu hadi 5.7 ifikapo mwaka ujao wa fedha.

Ameeleza nakisi ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha itafidiwa na fedha za nje ya nchi zinazochukua asilimia 2.7 ya Pato la Ndani (GDP) na fedha za ndani zinazochukua asilimia 3 ya Pato la Ndani. Na mapato ya kodi yataendelea kuongezeka kuendana na kufufuka kwa uchumi na mageuzi ya sera ya kodi na usimamizi wa mapato.

Wizara ya fedha ya Kenya pia imesema ili kudhibiti deni la serikali, serikali itasimamia na kudhibiti matumizi ya serikali.