Shirika la ndege la Tanzania lazindua safari nne za kikanda
2021-10-14 09:20:31| CRI

Shirika la ndege la Tanzania ATCL limetangaza kuwa litazindua safari nne mpya za kikanda kuanzia mwezi Novemba.

Ofisa wa mawasiliano wa shirika hilo Bw. Josephat Kagirwa amesema mjini Dar es Salaam kuwa safari hizo ni pamoja na Bujumbura Burundi, Ndola Zambia, Lubumbashi DRC na Nairobi Kenya.

Wiki iliyopita, Tanzania ilipokea ndege mpya zilizonunuliwa kutoka kwa watengenezaji wa Canada, zikiifanya idadi ya jumla ya ndege zinazomilikiwa na shirika hilo kuongezeka hadi kufikia 11.