Kenya yataka juhudi zaidi zifanyike kupambana na vurugu za kijinsia
2021-10-14 09:27:29| CRI

Kenya inataka juhudi zaidi zifanyike ili kukabiliana na changamoto za kijamii zinazotokana na ukatili wa kingono na vurugu za kijinsia (SGBV) nchini humo.

Mke wa Rais wa Kenya Bibi Margaret Kenyatta alipohutubia kwenye sherehe ya uzinduzi wa hati maalumu ya kukabiliana na vurugu za kijinsia iliyotolewa na Ofisi ya Polisi ya Kenya (Policare), amesema mapambano dhidi ya vurugu hizo yanahitaji juhudi za pamoja katika kuinua kiwango cha ufahamu wa umma na kutekeleza vizuri sheria husika, ili wahanga wajisikie salama wanaporipoti uhalifu dhidi yao. Pia ameongeza kuwa mila, desturi na imani zinazoweza kurudisha nyuma juhudi hizo na kusababisha uhalifu, zingechukuliwa hatua ili zimalizwe.

Policare ambayo ni sehemu ya mageuzi ya huduma ya polisi, inalenga kutoa huduma ya kituo-kimoja nchini kote kwa wahanga wa vurugu za kijinsia.