Kikundi cha tisa cha wataalamu wa afya wa China chaanza kazi nchini Sudan Kusini
2021-10-14 08:56:36| CRI

Kikundi cha tisa cha wataalam wa afya wa China ambacho kiliwasili hivi karibuni nchini Sudan Kusini tayari kimeanza kazi nchini humo.

Bw. Isaac Maker ambaye ni mkuu wa Hospitali ya mafunzo ya Juba watakapofanya kazi wataalam hao, amepongeza kikundi kilichomaliza muda wake na kikundi cha sasa kwa mchango mkubwa waliotoa kwenye maendeleo ya sekta ya afya ya Sudan Kusini.

Bw. Maker amesema wataalamu hao wanaisaidia sana hospitali hiyo, na wanatoa mchango mkubwa kwenye usimamizi wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Dk. Ding Zhen, tabibu mkuu na kiongozi wa kikundi cha tisa cha wataalamu wa afya wa China, amesema uwepo wao nchini Sudan Kusini unawawezesha kuwahudumia watu wa Sudan Kusini, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.