China yatangaza wanaanga wa chombo cha Shenzho-13, ikiwa ni pamoja na mwanamke wa kwanza kwenye kituo cha anga ya juu
2021-10-15 09:21:26| CRI

China imetangaza wanaanga watatu watakaokwenda kufanya kazi na kuishi kwenye kituo cha anga ya juu cha China kwa muda wa miezi sita, mmoja wao akiwa ni mwanamke.

Idara ya mpango wa chombo cha anga ya juu kinachobeba binadamu ya China imesema chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-13 kitarushwa kesho usiku kwa saa za Beijing kutoka kituo cha kurushia satellite cha Jiuquan. Wanaanga watakaopelekwa na chombo hicho watafanya kazi kwa muda wa miezi sita ambao ni muda wa kawaida kuishi na kufanya kazi kwenye kituo hicho.

Kwa sasa vyombo viwili vya anga ya juu vya kubeba mizigo vimetangulia kupeleka mahitaji, vikisubiri ujio wa wanaanga hao watakaokwenda.