Rais wa China apongeza kufunguliwa kwa Maonyesho ya 130 ya Biashara ya Kimataifa ya China
2021-10-15 10:02:56| cri

Rais Xi Jinping wa China ameandika barua ya pongezi kwa Maonyesho ya 130 ya Biashara ya Kimataifa ya China (Canton Fair) yaliyofunguliwa jana mjini Guangzhou, China.

Rais Xi amesema kwenye barua hiyo kuwa tangu maonyesho hayo yazinduliwe miaka 65 iliyopita, yametoa mchango mkubwa katika kuhudumia biashara ya kimataifa na kuhimiza mawasiliano ndani na nje.

Maonyesho hayo pia yanaendelea kuvumbua muundo mpya ya maendeleo na kupanua uwezo wake ili kujijenga kuwa jukwaa muhimu la China kufungua mlango kwa nje, kuhimiza maendeleo yenye ubora ya biashara ya kimataifa na kuunganisha mizunguko miwili ya ndani na nje ya nchi.

Amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, ikishikilia kuendeleza mifumo ya pande nyingi na kuhimiza kujenga uchumi wa dunia ulio wazi wa kiwango cha juu.