Kesi ya pili ya maambukizi ya Ebola yaripotiwa DRC
2021-10-15 09:52:54| CRI

Ofisi ya afya ya mkoa wa Kivu ya kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imeripoti mtu wa pili aliyeambukizwa virusi vya Ebola.

Mtu wa kwanza aliyethibitishwa alikuwa mvulana mdogo aliyekufa tarehe 6 mwezi Oktoba katika kituo cha afya huko Beni, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Ofisa mkuu wa afya wa Beni Bw. Michel Tosalisana amesema mtu wa pili ni mwanamke mwenye umri wa miaka 42 ambaye alithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Idara ya afya ya mkoa wa Kivu Kaskazini ilianza kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola chini ya msaada wa Shirika la Afya Duniani (WHO).