WHO kupeleka wataalamu ili kuzuia ukatili wa kingono baada ya kashfa ya DRC
2021-10-18 14:34:37| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa na shinikizo kubwa baada ya wafanyakazi wake kadhaa kutuhumiwa kuhusika na ukatili wa kingono nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

WHO Ijumaa limebainisha baadhi ya sera zake zilizoboreshwa za kuwawajibisha wafanyakazi pamoja na kuzuia kesi za ukatili wa kingono. Shirika hilo lilijikuta likikalia kaa la moto baada ya kutolewa ripoti inayoonesha baadhi ya wafanyakazi wake wamefanya vitendo vya ukatili wa kingono nchini DRC. Hivyo WHO inapanga kupeleka wataalamu ambao ni wajuzi wa kuzuia ukatili wa kingono na wanafahamu utamaduni wa nchi ambazo watapelekwa.