Familia 2,500 za wakulima zaanza mafunzo ya vitendo katika mashamba darasa ya FAO nchini Angola
2021-10-18 09:02:22| cri

 

 

Mratibu wa miradi ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika mkoa wa Cunene nchini Angola, Bw. Humberto Alves hivi karibunbi amesema, karibu familia 2,500 za wakulima katika mkoa wa kusini wa Cunene nchini Angola zimeanza mafunzo ya vitendo katika mashamba darasa yanayoendeshwa na Shirika hilo.

Akizungumza na wanahabari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani tarehe 16 mwezi huu, Bw. Alves amesema, FAO limeanzisha mashamba darasa 74 mkoani Cunene katika miezi 10 iliyopita.

Amesema utekelezaji wa mashamba darasa ni sehemu ya Mradi wa Kuimarisha Unyumbufu na Usalama wa Chakula na Lishe(FRESAN), ambao unalenga kupunguza uhaba wa chakula kwa watu wanaoishi kusini mwa Angola walioathiriwa sana na ukame.