Mfuko wa Wanyamapori Afrika wapongeza ahadi ya China kuunga mkono ulinzi wa viumbe hai
2021-10-18 08:18:44| CRI

Mfuko wa Wanyamapori wa Afrika umepongeza ahadi ya fedha iliyotolewa na China ya kuunga mkono ulinzi wa viumbe hai, ahadi iliyoonyesha nia yake ya kuboresha afya ya dunia.

Katika Mkutano wa 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Viumbe Anuwai wa Umoja wa Mataifa (COP 15) mjini Kunming, Yunnan, kusini magharibi mwa China, nchi hiyo ilitangaza pendekezo la kuanzisha mfuko wa anuai ya viumbe na kuchukua nafasi ya uongozi kwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 233 kuunga mkono ulinzi wa viumbe hai katika nchi zinazoendelea.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Kaddu Sebunya amesema kwenye taarifa yake kuwa, ahadi hiyo ya China, pamoja na zile za wadau wengine, ni mwanzo wa ukusanyaji wa rasilimali muhimu katika kutimia pengo la fedha katika ufadhili wa anuai ya viumbe.

Amesema wazo la China la ustaarabu wa kiikolojia litakuwa na athari chanya katika juhudi za kimataifa za kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi yanaenda sambamba na masikilizano na asili.