DRC kuanzisha Shirika jipya la Ndege la kitaifa
2021-10-18 08:18:11| CRI

Wizara ya Uchukuzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema, nchi hiyo inajiandaa kuanzisha kampuni mpya ya usafiri wa anga inayoitwa “Air Congo”.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Wizara hiyo imesema kampuni hiyo mpya itatumia ndege zenye ubora wa juu, na hii inatokana na kuingia ubia na Shirika la Ndege la Ethiopia, na kuongeza kuwa, Ethiopian Airlines itatoa ndege saba kwa DRC kama sehemu ya ubia huo.

Upatikanaji wa ndege hizo ni matokeo ya Makubaliano ya Awali yaliyosainiwa Septemba mwaka huu mjini Addis Ababa, Ethiopia, kati ya DRC na Shirika la Ndege la Ethiopia, ambapo DRC itakuwa na asilimia 51 ya hisa na kampuni hiyo ya Ethiopia kuchukua asilimia 49.