DRC yalishtumu jeshi la Rwanda kwa “uvamiazi”
2021-10-19 08:46:23| cri

 

 

     Msemaji wa jeshi la mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Guillaume Njike amesema, nchi hiyo inavishutumu vikosi vya Rwanda kwa "kuvamia" vijiji sita kaskazini mashariki mwa DRC Jumatatu asubuhi.

Msemaji huyo amesema, tangu jana asubuhi, jeshi la Rwanda limevamia eneo la Kibumba, mkoani Kivu Kaskazini, na kusababisha mapambano kati ya vikosi vya DRC na jeshi la Rwanda.

Ameongeza kuwa jeshi la Rwanda lililazimishwa kurudi nyuma kutokana na kupelekwa askari wa ziada wa DRC katika eneo hilo.

Jeshi la Rwanda bado halijajibu tukio hilo, lakini balozi wa Rwanda nchini DRC amekanusha uvamizi wowote.