Idadi ya vifo kutokana na shambulizi la silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria yafikia 43
2021-10-19 08:29:00| CRI

Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi lililofanywa na watu wenye silaha mkoani Sokoto, kusini magharibi mwa Nigeria imeongezeka na kufikia 43 kufuatia miili zaidi kupatikana.

Gavana wa mkoa wa Sokoto Aminu Waziri Tambuwal amesema jana jioni kuwa, kundi la wahalifu lilifanya shambulizi jumapili usiku katika mji wa Goronyo na kuua watu 43. Gavana huyo ametaka vikosi zaidi vya usalama vipelekwe mkoani humo ili kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Katika taarifa yake, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amelaani vikali shambulizi hilo, akisema siku za watu waliohusika na tukio hilo zinahesabika. Amesema wahalifu kwa sasa wako chini ya shinikizo kubwa kutokana na operesheni kali za anga na ardhini zinazofanywa na jeshi la Nigeria dhidi yao na maficho yao.