Uganda na China zatimiza miaka 59 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia
2021-10-19 08:30:15| CRI

Uganda na China jana jumatatu zimeadhimisha miaka 59 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Jeje Odongo amesema, ahadi ya nchi hiyo itaendelea kushikilia mshikamano, ushirikiano wa kunufaishana, ustawi na kutafuta amani na utulivu.

Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii, Ubalozi wa China nchini Uganda umesema, uhusiano wa pande mbili kati ya nchi hizo unaendelea kuimarika, na umefikia wakati mzuri wa kihistoria, ukiwa na matumaini mazuri ya kuendelea zaidi.

Mwaka 2019, nchi hizo mbili zilikubaliana kuongeza ngazi ya uhusiano wao na kufikia ushirikiano wa kina wa pande zote, pia nchi hizo zinafanya kazi pamoja katika kutekeleza Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja pamoja na matokeo ya Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) uliofanyika hapa Beijing Septemba, 2018.