DRC yaripoti kesi tatu mpya za Ebola
2021-10-19 08:45:39| cri

DRC yaripoti kesi tatu mpya za Ebola_fororder_VCG211240254601

Kesi tatu mpya za virusi vya Ebola zimethibitishwa na maafisa wa afya katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani(WHO) huko DRC ilisema Jumatatu kwenye ukurasa wa Twitter kuwa, mpaka kufikia jumamosi iliyopita, kesi tatu mpya zilithibitishwa, ikiwemo vifo vya wagonjwa wawili katika eneo la Butsili mjini Beni, na kufikisha jumla ya kesi tano na vifo vitatu nchini humo.

Oktoba 8, Wizara ya afya nchini DRC ilitangaza kuibuka upya kwa virusi vya Ebola katika mkoa wa Kivu Kaskazini, bila ya kutoa taarifa zaidi, ikiwa ni miezi mitano baada ya kumalizika kwa mlipuko mwingine wa Ebola katika eneo hilo.