Somalia na Umoja wa Mataifa zafikiria njia za kuboresha mfumo wa chakula
2021-10-20 08:30:35| CRI

Somalia na Umoja wa Mataifa zimetoa wito wa kuchukua hatua za kuboresha mifumo inayohusika na uzalishaji na usambazaji wa chakula nchini humo.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji ya Somalia zimesema, katika miaka michache iliyopita, Somalia imeshuhudia majanga yanayojitokeza mara kwa mara ikiwemo uvamizi wa nzige wa jangwani na mafuriko pamoja na ukame, ambavyo vinaathiri mfumo wa uzalishaji na maisha ya watu.

Waziri wa wizara hiyo Said Hussein Iid amesema, serikali ya Somalia inatoa kipaumbele katika kuanzisha mazingira mazuri kwa ajili ya mifumo imara na endelevu ya chakula nchini humo.