Kurejeshwa kwa kiti cha China katika Umoja wa Mataifa ni hatua kubwa kimataifa
2021-10-20 08:31:05| CRI

Mratibu Mkazi wa Mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini China Siddharth Chatterjee amesema, maadhimisho ya miaka 50 tangu kurejesha kiti cha China katika Umoja wa Mataifa ni ishara ya hatua kubwa sio tu kwa China, bali kwa dunia nzima.

Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Chatterjie ameipongeza na kuisifu China kwa mafanikio yake katika miaka 50 iliyopita, na kuisifu nafasi ya China kama nchi mwanachama wa pande nyingi, na mwongozaji muhimu katika anga ya Umoja wa Mataifa.

Amesema mafanikio ya China hayawezi kupuuzwa, na kuongeza kuwa, Benki ya Dunia imesema kuwa katika miaka 25 iliyopita, hatua ya China ya kuondoa watu wake kutoka umasikini imekuwa na athari kubwa katika Lengo la Kwanza la Maendeleo Endelevu (SDG 1), ambalo ni kuondokana na umasikini.