Watoto watatu wauawa katika shambulizi la anga nchini Ethiopia
2021-10-20 08:30:04| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, watoto watatu wameuawa na watu wengine 10 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya anga yaliyotokea jumatatu mjini Mekelle, mji mkuu wa mkoa wa Tigray nchini Ethiopia.

Haq ameelezea kuongezeka kwa mashambulizi kuwa ni jambo la kuleta wasiwasi, na kwamba Umoja wa Mataifa unazitaka pande zote husika kukumbuka wajibu wao chini ya Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu na kulinda raia na miundombinu yao.

Pia amesema, uhaba wa mahitaji muhimu, hususan mafuta na fedha, unavuruga operesheni za kibinadamu katika mkoa wa Tigray, na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikishwa kwa wahitaji.