Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Ethiopia kuanza shahada ya uzamili ya lugha ya Kichina
2021-10-20 09:10:21| CRI

Chuo Kikuu cha Addis Ababa, Ethiopia kuanza shahada ya uzamili ya lugha ya Kichina_fororder_540096fd066b445c9a4c50704e50ce78

Chuo Kikuu cha Addis Ababa cha Ethiopia kimekamilisha maandalizi ya kuanzisha shahada ya uzamili ya lugha ya Kichina utakaotekelezwa kwa msaada wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu hicho.

Naibu mkuu wa taaluma wa Chuo Kikuu hicho Emebet Mulugeta amesema, masomo ya shahada ya uzamili ya lugha ya Kichina nchini Ethiopia yataleta nguvu inayohitajika katika kueneza lugha ya Kichina nchini Ethiopia na kukuza uhusiano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa ilizinduliwa mwaka 2012, na hadi sasa imesajili zaidi ya wanafunzi 10,000, kati yao, zaidi ya 100 wamepata shahada ya kwanza ya lugha ya Kichina.