Mwandishi maalumu wa UM akutana na rais wa Zimbabwe kuhusu athari za vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi
2021-10-20 08:31:46| CRI

Mwandishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari hasi ya hatua za lazima zilizochukuliwa kwa upande mmoja kwa haki za binadamu, Alena Douhan, jana amewasili Zimbabwe kwa ziara ya siku 10 ili kutathmini athari za vikwazo dhidi ya Zimbabwe.

Akiwa nchini humo, Douhan amekutana na rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana kabla ya kukutana na wadau wengine ambapo atakukusanya taarifa kuhusu athari hasi ya vikwazo hivyo.

Rais Mnangagwa amesisitiza kuwa, vikwazo vya nchi za magharibi vinaumiza raia wa Zimababwe.

Ikiwa sehemu ya kazi yake, Douhan atatembelea maeneo kadhaa ili aweze kutathmini athari za vikwazo kabla ya kutoa mapendekezo na miongozo ya kupunguza au kuziondoa athari hizo.