Wapalestina 17 wajeruhiwa kwenye mgogoro huko Jerusalem Mashariki
2021-10-20 08:34:45| cri

Wapalestina 17 wajeruhiwa kwenye mgogoro huko Jerusalem Mashariki_fororder_VCG111353885444

Wapalestina 17 wamejeruhiwa, 10 kati yao vibaya, baada ya kutokea mapambano kati ya raia wa Palestina na askari polisi wa Israel karibu na Mlango wa Damascus huko Jerusalem Mashariki.

Kwa upande wa Israel, dereva mmoja wa basi na abiria mmoja wamejeruhiwa. Polisi wa Israel wametoa taarifa wakisema, watuhumiwa 22 wamekamatwa.

Vyombo vya habari vya Israel vimesema, migogoro kati ya Israel na Palestina inatokea mara kwa mara karibu na Mlango wa Damascus katika siku kadhaa zilizopita, na makumi ya wapalestina wamekamatwa.