Serikali ya Ethiopia yathibitisha kufanya mashumbulizi ya anga mkoni Tigray
2021-10-21 08:51:31| CRI

Serikali ya Ethiopia jana imethibitisha kufanya mashambulizi ya anga katika mkoa wa Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Harakati za Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) lililokuwa likitawala mkoa huo, lililishutumu jeshi la nchi hiyo kwa kufanya mashambulizi ya anga yaliyolenga maeneo ya makazi ya raia.

Hata hivyo serikali ya Ethiopia imesema, tofauti na habari zilizotolewa, jeshi lake lililenga maeneo yanayotumiwa na TPLF kutengeneza silaha, na kuongeza kuwa, operesheni hizo zililenga kuharibu idadi kubwa ya silaha haramu katika maeneo husika.