Rais wa Tunisia apinga aina yoyote ya uingiliaji wa mambo ya ndani ya Tunisia
2021-10-21 08:58:07| cri

Rais Kais Saied wa Tunisia amesema, nchi yake inapinga aina yoyote ya uingiliaji wa nje.

Katika mazungumzo yake na katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Bw. Ahmed Aboul Gheit hapo jana, rais Saied amesema Tunisia inapenda kufanya mashauriano na ushirikiano na nchi nyingine rafiki kwa msingi wa kuheshimiana, na kusifu msimamo wa Bw. Gheit wa kuiunga mkono Tunisia.

Kwa upande wake, Bw. Gheit amesema, ana imani na mchakato wa kidemokrasia nchini Tunisia na hatua madhubuti zinazochukuliwa. Amemtaka kiongozi huyo wa Tunisia kutimiza utulivu na maendeleo wa kitaifa kulingana na matakwa ya watu.