Niger yapenda kuhimiza uhusiano kati yake na China
2021-10-21 09:43:42| cri

 

 

     Rais Mohamed Bazoum wa Niger jana amesema, nchi yake inapenda kufanya juhudi pamoja na China, na kuhimiza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

     Rais Bazoum amesema, ushirikiano kati ya Niger na China kwenye sekta za miundombinu, mafuta na afya umepata mafanikio makubwa, na kuwanufaisha wananchi wao. Niger inatilia maamani sana kuendeleza uhusiano na China, inaichukulia China kuwa mwenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa kuaminika, na inapenda kufanya juhudi pamoja na China ili kusonga mbele uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati yao.